Historia Fupi.


KLABU ya waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro (Morogoro Press Club) mchakato wa kuanzishwa mwaka 1996 ilipofika tarehe 13/3/1997 ikapata usajili Wizara ya Mambo ya ndani na kupata cheti cha usajili chenye namba. SO.NO.9009 ikiwa na wanachama 20 kwa sasa Morogoro Press Club ina wanachama 80.

Ofisi ya MOROPC ipo katika jengo la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Kata ya Kingo mkabala ya Mahakama ya mwanzo ya Nunge,Manispaa ya Morogoro.

VIONGOZI WA MOROGORO PRESS CLUB 2015-2018
Nickson Mkilanya-Mwenyekiti
Ashhton Balaigwa-Makamu Mw/kiti

Jonh Kidasi Katibu Mtendaji 

Jimmy Mengele-Katibu Msaidizi
 Merina Robert - Mweka hazina
Agness Haule - Mweka hazina msaidizi
 Severin Blasio-Mjumbe

Christina Haule - Mjumbe
Fadhil Rashid-Mjumbe

Thadei Hafigwa-Mratibu





MADHUMUNI NA MALENGO
 1. Ni chama cha kitaaluma malengo yake mahususi ni kujenga mahusiano miongoni mwa wanachama na makundi yenye makusudio tofauti ikiwa ni pamoja na taasisi za raia.

 2. Kuwa kitovu cha masuala ya waandishi wa habari katika mkoa wa Morogoro.

3. Kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafanyakazi kulingana na maadili ya waandishi wa habari kama ilivyofafanuliwa na Baraza la Habari.

4. Kuinua kiwango cha taaluma katika tasnia ya habari kwa kuendesha mafunzo mafupi mafupi kwa wanachama wake.

5. Kuwezesha wanachama kutumia rasilimali chache zilizopo katika kuboresha shughuli za ukusanyaji na usambazaji wa habari miongoni mwa waandishi wa Watanzania.

 6. Kuimarisha ushirikiano miongoni mwa waandishi wa habari,watoa habari na taasisi za kitaaluma zenye kulenga kuongeza ufanisi katika habari na mawasiliano kwa maanufaa ya wanachama wote na jamii na kuitangaza vema Mkoa wa Morogoro ili kusukuma maendeleo ya wananchi kwa kasi.

 7. Kuwalinda waandishi wa habari dhidi ya madai yenye mwelekeo wa kitaaluma.

DHAMIRA:"Kuwaimarisha waandishi wa habari Kitaaluma"

 DIRA:"Kuwa na jamii yenye uhuru wa kujieleza na Uhuru wa Habari"

 Morogoro Press Club kama ilivyo Taasisi nyingine mara baada ya kupata usajili wake ilipita katika hatua mbalimbali za uongozi.

Awamu ya kwanza 1997-2000
 Ndg.Anaclet Rwegayura-Mwenyekiti
 Bi.Halima Kihemba -Makamu Mwenyekiti
Ndg.Wilson Karuwesa- Katibu na mtunza fedha.

Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Ndg.Richard Mwangulube
Ndg.Said Mtaalamu
Ndg.Aziza Msuya.

Awamu ya pili 2001 hadi 2002
 Ndg Said Dogori Mwenyekiti
 Ndg.Bonventure Mtalimbo-Makamu Mwenyekiti
 Marehemu Aidan Libenanga-Katibu Mkuu
 Bi.Monica Lyampawe- Mtunza fedha.
  
Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Ndg.Simon Berege
 Ndg.Halfan Diyu
 Ndg.Richard Mwangulube.

 Awamu ya tatu 2002 hadi 2004.
Marehemu Seraph Kuandika-Mwenyekiti
Ndg.Bujaga Kadago- Makamu Mwenyekiti
Ndg.Sita Peter wake-Katibu Mkuu
Bi.Merina Robert- katibu Mkuu msadizi.
Bi.Kasilda Mgeni- Mtunza fedha.

Wajumbe watatu wa kamati ya tendaji
 Ndg.Nikson Mkilanya
 Ndg.Samweli Msuya
 Ndg.James Mkisi.

Awamu ya nne Julai 2004 hadi 2007.
 Ndg.Bonventure Mtalimbo- Mwenyekiti
 Bi.Idda Mushi- Makamu Mw/kiti.
 Ndg.Thadei Hafigwa- Katibu Mkuu
 Ndg.Said Mtaalam katibu mkuu msaidizi
 Ndg.Samweli Msuya- Mtunza fedha

 Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Marehemu Gilbert Suleman
 Ndg.Said Dogoli
.Ndg.Wilson Karuwesa
.
Awamu ya tano Julai 2007 hadi 2011
 Ndg.Bonventure Mtalimbo- Mwenyekiti
 Bi. Idda Mushi- makamu Mw/kiti
 Ndg.Thadei Hafigwa -Katibu Mkuu.
 Bi.Devota Minja K/Msaidizi
 Ndg.Samweli Msuya- Mtunza fedha

Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Ndg.Ramadhani Libenaga
 Ndg.Ashton Balaigwa
 Bi. Lilian Lucas

Awamu ya sita Novemba 2011-2014
 Ndg.Aziz Msuya-Mwenyekiti
Bi.Devota Minja-Makamu Mw/kiti
 Ndg.Abedi Dogoli-Katibu Mtendaji
 Bi.Lilian Lucas-Mwekahazina

 Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Bi.Latifa Ganzel
 Bi.Monica Liampawe
 Ndg.Venance George

Mabadiliko ya kimfumo
Mwaka 2011 Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania ambapo sisi ni miongoni mwa wanachama wake ulinda mfumo wa kuwa na waratibu wa Klabu katika mikoa yote wanaoajiliwa ili kuhakikisha ya kuwa shughuli zote za kiutendaji vinafanyika. Kwa mkoa wetu wa Morogoro nafasi hiyo inashirikiwa na Ndg.Thadei Hafigwa

 Mabadiliko ya kimifumo Awamu Saba Machi 2013-Agosti 2015
 Bi.Idda Mushi-Mwenyekiti
 Ndg Nickson Mkilanya-Makamu Mw/kiti
 Ndg.Abedi Dogoli-Katibu Mtendaji
 Ndg.Ramadhan Libenanga-Katibu msaidizi
 Bi.Lilian Lucas-Mwekahazina
Ndg.Peter Kimath-Mwekahazina Msaidizi

Wajumbe watatu wa kamati tendaji
 Ndg.Ashton Balaigwa
 Ndg.Fadhil Rashid
 Bi.Vaileth Mbwillo
 Ndg.Thadei Hafigwa-Mratibu

Awamu ya Nane Agosti 2015-Agosti 2018
 Ndg.Nickson Mkilanya-Mwenyekiti
 Ndg.Ashton Balaigwa-Makamu Mw/kiti
 Ndg.John Kidasi-Katibu mtendaji
Ndg.Jimmy Mengele-Katibu Msaidizi
 Bi.Merina Robert-Mwekahazina
 Bi.Agnes Haule-Mwekahazina Msaidizi

Wajumbe watatu wa Kamati tendaji
 Ndg.Fadhil Rashid
 Ndg.Severin Blasio
 Bi.Christina Haule

KAMATI YA MAADILI MOROGORO PRESS CLUB
 Jukumu la kamati hii ni kuhakikisha ya kuwa inasimamia masuala yote ya kitaaluma na kusuluhisha malalamiko kati ya waandishi wa habari na wadau pale inapojitokeza upande mmoja kuona haikutendewa haki
 Viongozi wa kamati hii ni÷
 Mzee Rashid Lusewa-Mwenyekiti kamati ya maadili
 Ndg.Saidi Dogoli-Mjumbe
Ndg. Bonventure Mtalimbo-Mjumbe
 Ndg.Wilson Karuwesa
 Sheikh Ally Omar-Mjumbe
 Rev.Fr.Makseyo-Mjumbe
Ndg.John Nyabinyiri-Mwanasheria
 Bi.Aziza Msuya-Mjumbe
 Ndg.Nickson Mkilanya-Mjumbe
 Ndg.John Kidasi-Mjumbe
 Ndg.Thadei Hafigwa-Mjumbe

 Pia Morogoro Press Club ina kamati ndogondogo za kusaidia kuharakisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Kamati ya mipango uchumi, fedha na Mahusiano
 Majukumu ya kamati hii ni kushirikiana na Kamati tendaji katika kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuhakikisha ya kuwa Klabu inapata mapato

Viongozi wa kamati hii ni
 Kasilda Mgeni-Mwenyekiti
 Latifa Ganzel-Katibu
 Merina Robert-Mwekahazina

 Kamati ya ujenzi na ustawi wa Jamii.
 Majukumu ya kamati hii ni kushirikiana na Kamati tendaji katika kutafuta mfumo wenye tija katika kuhakikisha ya kuwa Klabu inakuwa na  jengo la kitega uchumi.
 Pia kuhakikisha ustawi wa wanachama na jamii unaimarika hasa kwenye sherehe,ugonjwa na vifo kwa kuandaa mfumo maalum utakaosaidia malengo yaliokusudiwa yanafikiwa.

Viongozi wa kamati hii ni
 Monica Liampawe-Mwenyekiti
 Lilian Lucas-Katibu
 Agnes Haule-Mwekahazina.
 Mkoa wa Morogoro una waandishi zaidi ya 100 ambao wanajumuisha wanachama wa Morogoro Press Club,na wasio  wanachama ambao wanaofanyakazi katika vyombo mbalimbali vya habari vya serikali na binafsi.
 Mlezi wetu wa Morogoro Press Club ni Mkuu wa Mkoa Mstaafu,Mhe.Stephen Joshua Mashishanga

MAFANIKIO YA MOROPC

Miongoni mwa mafanikio yaliopatikana ni pamoja na
1. Kuweza kupaza sauti kwa wasio na sauti.
2. Kuwa kiungo kati ya serikali na wananchi(people centered)
3. Imeweza kujiunga na taasisi za kitaaluma kama vile Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na Baraza la Habari Tanzania(MCT).
4. Kutokana na kuwa mwanachama wa taasisi hizo MOROPC kimenufaika vitendea kazi(vifaa vya ofisi na samani) kama kompyuta, TV, Printer,scanner,kamera ya picha za mnato na picha za video(moving)
5. Pia wanachama wanapata mafunzo na semina za kitaaluma katika kukumbusha masuala yote ya kimaadili.wanachama wanapata machapisho mbalimbali ya kitaaluma.
6. Kuwa na blog yenye lengo la kuwahabarisha jamii kazi na majukumu mbalimbali ya  taaluma ya habari.
7. Kuanzisha mfumo maalum wa kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kijamii(bima ya afya,)

MIKAKATI YA KLABU.

 Pamoja na mafanikio yote hayo pia MOROPC ina mikakati ya muda mrefu na muda mfupi,ikiwa ni pamoja na kumiliki jengo lake la kitega uchumi ili kuwa na uandishi wa habari wa kiuchumi.

Morogoro Press Club ipo katika mchakato wa kuanzisha gazeti la Klabu kwa ajili ya kupanua wigo wa kuwahudumia wananchi wa maeneo yote mjini na vijijini ikiwa ni fursa yao kutoa maoni,changamoto na mafanikio wanayoyapata katika shughuli zao za kiuchumi,Kijamii na kiutamaduni.

MAHUSIANO NA TAASISI ZINGINE

MOROPC imekuwa na mahusiano na Taasisi za ndani na nje ya nchi AkibaUhaki foundation iliopo Nchini Kenya,Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzani(UTPC) na Baraza la Habari Tanzania(MCT).

CHANGAMOTO
 Morogoro Press Club haina jengo lake la ofisi inategemea zaidi kupanga na wakati mwingine kushindwa kutimiza majukumu yetu ya kuwahudumia wananchi katika kiwango chenye ufanisi.

 MOROPC inakabiliana na changamoto ya raslimali fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango mkakati ya kuimarisha taasisi na wanachama wake.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni